Tatizo la mawe kwenye figo (kidney stones)-2

Blausen_0595_KidneyStones.pngNi siku nyingine tena, na ni imani yangu mu wazima wa afya njema wapenzi wasomaji wangu wa makala hii. Wiki iliyopita hatukumaliza kuzungumzia tatizo la mawe kwenye figo (kidney stones), leo tunaendelea na sehemu ya mwisho, fuatana nami.

Ulaji wa matunda ni njia mojawapo inayosaidia kuepukana na tatizo hili, matunda kama vile tikiti maji, mananasi na matunda mengine yanayopunguza sumu mwilini yanamchango mkubwa sana katika kumwepushia mtu kukumbwa na tatizo la mawe kwenye figo.

Pia matunda yenye uwezo mkubwa wa kutoa kinga na hata nafuu kwa mgonjwa wa mawe kwenye figo ni pamoja na tufaa (apple) ambalo lina kirutubisho aina ya ‘pectin’ ambacho kina uwezo wa kulainisha na kuyeyusha mawe na kuzuia mengine kujitengeneza kwenye figo. Pia juisi za limao, machungwa (jamii zote), hutoa kinga imara dhidi ya ugonjwa huu hatari.

Pia matumizi ya juisi halisi za matunda (ya kutengeneza nyumbani, siyo viwandani) pamoja na mboga za majani kwa wingi. Juisi na mboga za majani huondoa mrundikano wa uchafu na sumu katika kibofu na figo hivyo kuuacha mwili wako salama.

Niwakumbushe tu wasomaji kuwa tatizo hili linatibika kwa kutumia mimea tiba mbalimbali  ambayo imechanganywa kwa njia za asili bila kemikali. Lakini kama una tatizo hili na unajisikia aibu kumweleza mwenzi wako tupigie simu katika namba zetu au tutembelee Sigwa Herbal Clinic katika vituo vyetu vilivyopo Dar es Salaam, Mbeya, Njombe, Singida, Kahama, Moshi, Morogoro, Dodoma, Arusha, Tanga, Kigoma, Mwanza na Bukoba.


Loading...

Toa comment