The House of Favourite Newspapers

Tatizo la mawe kwenye figo (Kidney Stones)

FIGO ni kiungo muhimu katika mwili wa binadamu, hufanya kazi ya kuchuja damu huku ikiondoa sumu zote za mwili, figo hufanya kazi ya kurekebisha kiasi cha maji mwilini (electrolyte level).

Kabla damu haijapita katika figo, huwa imebeba maji na takataka nyingi sana (urea), lakini inapopita katika figo huchujwa na vitu muhimu hurudishwa katika mzunguko wa damu lakini masalia mengine ambayo hayafai tena katika mwili ikiwa ni pamoja na kiwango cha maji kilichozidi, hupitishwa kwenye mirija miwili kitaalamu iitwayo ureters kuelekea kwenye kibofu kitaalamu urinary bladder na kisha kutolewa nje ya mwili kupitia njia ya mkojo (urethra).

Mkusanyiko wa kemikali hizi wakati mwingine hugandamana na kutengeneza chembechembe ya vitu kama mchanga, kadri siku zinavyozidi kuendelea ndivyo vinavyozidi kukua hadi hufikia hatua ya kuziba njia ya mkojo katika figo yenyewe (neprone) au kwenye mirija ya kupeleka mkojo kutoka kwenye figo kwenda kwenye kibofu (ureteter), hapo ndipo mtu anaanza kupata shida ya kukojoa na kusikia maumivu makali.

DALILI ZA UWEPO WA MAWE

Mtu mwenye mawe kwenye figo huonyesha dalili zifuatazo; Maumivu ya mgongo na kiuno, mkojo kutoka ukiwa na rangi ya damu, kutokwa na jasho wakati wa usiku na kupatwa na homa kali kwa wakati flani ikiambatana na kutetemeka mwili.

Dalili nyingine ni kuhisi kichefuchefu na kutapika, mkojo kuwa na harufu kali, maumivu makali sehemu za mbavu, miguu kujaa maji/ kuvimba, maumivu ya tumbo chini ya kitovu upande wa kushoto au kulia kutegemea ni figo ya upande gani iliyoathirika na maumivu makali unapogusa upande wa figo iliyoathirika.

KISABABISHI CHA MAWE KATIKA FIGO

Mtu hupata mawe kwenye figo (Kidney stones); ikiwa kutokana na matumizi ya baadhi ya dawa, husababisha mtu kupata mawe katika figo pindi anapozitumia kila mara.

Dawa hizo ni kama vile za kutibu kansa na HIV, antibiotic kama ciprofloxacin, cefrtriaxone na madawa yenye sulphur kama metacalphin nk.

Pia utumiaji wa vyakula vyenye kuongeza vitamin A na D, ambavyo huongeza kwa kiasi kikubwa madini joto mwilini, kuishi kwenye mazingira ya joto sana bila kupata maji ya kutosha husababisha kiasi cha chemical kuongezeka katika figo na kusababisha zigandamane na kutengeneza mawe ndani ya figo.

Itaendelea wiki ijayo.

Comments are closed.