TATIZO LA MAWE KWENYE FIGO

UGONJWA wa mawe kwenye figo siyo mgeni miongoni mwa watu hivi sasa. Hata hivyo, katika siku za hivi karibuni, ukubwa wa tatizo hili umeongezeka, kwani hata vijana wanapatwa na tatizo hili ambalo kitalaam linajulikana kama Gallstones.

 

Figo ni kiungo muhimu katika mwili wa binadamu, hufanya kazi ya kuchuja damu huku ikiondoa sumu zote za mwili, figo hufanya kazi ya kurekebisha kiasi cha maji mwilini.

 

Kabla damu haijapita katika figo, huwa imebeba maji na takataka nyingi sana (urea), lakini inapopita katika figo huchujwa na vitu muhimu hurudishwa katika mzunguko wa damu, lakini masalia mengine ambayo hayafai tena katika mwili ikiwa ni pamoja na kiwango cha maji kilichozidi hupitishwa kwenye mirija miwili (ureters) kuelekea kwenye kibofu (urinary bladder) kisha kutolewa nje ya mwili kupitia njia ya mkojo (urethra).

 

Mkusanyiko wa kemikali hizi (chemical crystals), wakati mwingine hugandamana na kutengeneza chembechembe ya vitu kama mchanga, kadiri siku zinavyozidi kuendelea ndivyo vinavyozidi kukua hadi wengine hufikia hatua ya kuziba njia ya mkojo  katika figo yenyewe au kwenye mirija ya kupeleka mkojo kutoka kwenye figo kwenda kwenye kibofu (ureteter).

Hapo ndipo mtu anaanza kupata shida ya kukojoa na kusikia maumivu makali. Mawe ya kwenye figo siyo mawe halisi, bali huwa ni vitu vinavyojitengeneza kwenye figo taratibu na baada ya muda mrefu hugeuka umbo na kuwa mfano wa vijiwe vidogo na wakati mwingine huwa vikubwa mfano wa dole gumba.

 

DALILI ZA UGONJWA

Dalili za awali za mtu mwenye mawe kwenye figo ni maumivu ya wastani au makali ya tumbo ya mara kwa mara. Pia mtu mwenye uwezekano wa kuwa na mawe kwenye figo huwa na tatizo la ukosefu wa choo kwa muda mrefu, tumbo kujaa gesi, kujisikia kushiba sana baada ya kula chakula kidogo na kujisikia kichefuchefu mara kwa mara.

 

Aidha, mtu mwenye tatizo la mawe kwenye figo, huwa hapatani na vyakula vyenye mafuta mengi, kwani anapokula hujisikia vibaya zaidi, husumbuliwa na kizunguzungu, hupungukiwa damu mwilini na kuota chunusi usoni kwa wingi.

 

Tatizo la kuwa na mawe kwenye figo, husababishwa zaidi na ulaji mkubwa wa vyakula vyenye mafuta mengi na vyakula vinavyopikwa kutokana na unga mweupe (uwe wa mahindi, ngano au mchele) ambao huondolewa viini lishe vyake vyote. Pia ulaji mkubwa wa sukari kwa njia mbalimbali, kama vile juisi, soda, chai, keki, ice creams, n.k. Huweza kusababisha tatizo la mawe kwenye figo.

 

Kwa kawaida, kiwango cha sukari kinachotakiwa mwilini ni kile kisichozidi gramu 25 (sawa na kijiko kimoja kidogo cha chai) kwa siku, lakini kutokana na vyakula na vinywaji tunavyokunywa kwa siku, tunazidisha zaidi ya mara kumi ya kiwango cha kawaida.

 

Ukiwa na staili ya maisha hayo, ujue uko hatarini kupatwa na tatizo kama hilo. Kwa kina mama, ulaji wa muda mrefu wa vidonge vya uzazi wa mpango, nao husababisha tatizo. Kwa upande wa unga wa mahindi na ngano, tunapenda kutumia unga mweupe ambao umeshaondolewa viini lishe vyake vyote hivyo kukosa faida mwilini zaidi ya kufanya usagaji wa chakula tumboni kuwa mgumu na kusababisha ukosefu wa choo kwa muda mrefu.

 

Kitendo cha kukosa choo kwa muda mrefu wakati unakula na kunywa kila siku, ni dalili tosha kwamba vyakula unavyokula havina viini lishe na hivyo uko hatarini kupatwa na matatizo kwenye figo yako. Vilevile mtu kutokuwa na tabia ya kunywa maji mengi kila siku, huchangia ukosefu wa choo na matatizo kwenye figo.

 

MATIBABU

Tiba ya tatizo la mawe kwenye figo, mara nyingi huwa ni upasuaji wa kuvitoa na hugharimu fedha nyingi.

KINGA NA USHAURI

Mtu unaweza kujikinga ili usipatwe na mataizo kwenye figo kwa kujiepusha na ulaji wa vyakula visivyokuwa na lishe. Weka tabia ya kula mboga za majani na matunda ya aina mbalimbali kila siku, pendelea kula ugali wa dona badala ya sembe nyeupe, epuka mazoea ya kuweka sukari nyingi kwenye chai au vinywaji vingine vinavyotumia sukari.

 

Unashauriwa kunywa maji zaidi ya lita 2 hadi 5 kila siku ili kuepuka mawe kutengenezeka kwenye figo. Maji ndiyo husafisha seli na kuondoa sumu na kemikali zinazojitengeneza mwilini kuwa mawe.

 

Epuka unywaji wa soda kila siku, kwani unapokunywa soda moja tu, unakuwa umezidisha sukari mwilini mara sita ya kiwango kinachotakiwa. Kuwa na tabia ya kunywa maji mengi kila siku (angalau lita 2 hadi 5) hata kama husikii kiu, maji husaidia kusafisha figo pale unapoenda haja ndogo. Ni vema kama utaona dalili tulizozitaja hapa uwahi kumuona daktari.

Toa comment