The House of Favourite Newspapers

Tatizo Lazikumba Whatsapp, Facebook na Instagram

 

MTANDAO wa kijamii wa Facebook kwa sasa unapitia hali mbaya zaidi ya mawasiliano kuwahi kutokea katika historia yake kwani huduma nyingi hazipatikani kote ulimwenguni.

 

“Tunafahamu kuwa baadhi ya watu hawana na hawawezi kufikia app zinazohusiana na Facebook ,” ilisema taarifa iliyotolewa na Facebook.

 

“Haijabainika wazi ni nini kinachosababisha shida hiyo.  Tunafanya kila juhudi kushughulikia tatizo lililopo haraka iwezekanavyo,”

 

Mbali na Facebook yenyewe, huduma za Messenger na Instagram zimekumbwa na matatizo pia.

 

Mara ya mwisho Facebook kujikuta katika hali hiyo ilikuwa mwaka 2008 wakati mtandao huo ulikuwa na watumiaji milioni 150,  ikilinganishwa na sasa ambapo watumiaji wanakadiriwa kuwa karibu bilioni 2.3 kwa mwezi.

 

Kampuni ya Facebook imejibu uvumi unaoendelea mitandaoni kuwa huenda mtandao huo maarufu duniani umedukuliwa.

 

Inasema hali hiyo haijatokana na shambulio lolote la kimtandao. Inakadiriwa kuwa tatizo hilo lilianza kuukumba mtandao huo siku ya Jumatano.

 

Japo huduma ya Facebook ilionekana kuwa sawa, watumiaji wake waliripoti kuwa hawawezi kutuma ujumbe.

 

Watumiaji wa Instagram hawawezi kufikia ujumbe mpya huku wale wanaotumia huduma ya Facebook Messenger kupitia kompyuta pia wanakabiliwa na changamoto sawa na hiyo.

 

Hata hivyo, watumiaji wa mtandao huo kupitia app ya simu waliweza kutuma baadhi ya ujumbe japo nao pia walielezea kupata changamoto ya kutuma picha.

 

 

Mtandao wa WhatsApp, pia uliathiriwa na changamoto hizo. Hali hiyo imeathiri kampuni zinazotumia Facebook kuendesha biashara zao kwa sababu walishindwa kabisa kuwasiliana.

 

Mwana mitindo Rebecca Brooker ambaye anatumia mtandao huo kufanya kazi zake jijini Buenos Aires, ameliambia shirika la utangazaji la Uingereza (BBC),  kuwa hali hiyo imeathiri vikubwa biashara yake.

 

“Facebook kwa matumizi ya kibinafsi ni sawa lakini kwa kampuni kubwa zinazoendesha huduma zao kupitia mtandao huo,  unatarajia hii inamaanisha nini kwao?” alisema.

 

Nchini Uingereza mshauri na mtaalamu wa magonjwa ya watoto aliiambia BBC kuwa wafanyakazi wenzake walisikitika kwa kukatizwa kwa huduma hizo kwa sababu walikuwa na hafla ya kumuaga muuguzi mmoja ambaye amehudumu kwa miaka 20.

 

“Ilikuwa siku ya kazi na washauri wengi hawakuweza kufika lakini walitegemea kutumia whatsApp kujumuika pamoja,” alisema Dr Nikhil Ganjoo.

 

“Kwa hivyo nililazimika kuwakilisha lakini sikuweza hata kuwatumia picha za matukio katika hafla hiyo.  Tatizo hilo linatokea wakati wabunge nchini Marekani wanatafakari uwezekano wa kuyavunjilia mbali makampuni makubwa ya teknolojia – si  Facebook tu.

Comments are closed.