Rais Samia Apiga Kura Chamwino, Asimama Kwenye Foleni Na Wananchi Wengine – Video
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amepiga kura kwa ajili ya kuchagua viongozi kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mtaa katika kitongoji cha Sokoine, Chamwino mkoani Dodoma tarehe 27 Novemba, 2024.