TAZAMA LIVE: Mwili wa Mbunge Macha wa Chadema Waagwa Bungeni – Dodoma

DODOMA: Spika wa Bunge, Job Ndugai, ameongoza waombolezaji kuaga mwili wa Marehemu Dkt Elly Marko Macha Mbunge wa Viti Maalum-CHADEMA katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.

Dkt. Macha alifariki dunia Machi 31, 2017 katika Hospitali ya New Cross nchini Uingereza alikokuwa akitibiwa.

Macha aliyekuwa mlemavu wa macho tangu akiwa mtoto wa miezi mitano, amefariki akiwa na umri wa miaka 55 (1962-2017).

Baada ya kuaga mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda nyumbani kwake Moshi mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi.


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment