TAZAMA LIVE: Mwili wa Mbunge Macha wa Chadema Waagwa Bungeni


Imewekwa na on April 21st, 2017 , 10:38:23am

TAZAMA LIVE: Mwili wa Mbunge Macha wa Chadema Waagwa Bungeni – Dodoma

DODOMA: Spika wa Bunge, Job Ndugai, ameongoza waombolezaji kuaga mwili wa Marehemu Dkt Elly Marko Macha Mbunge wa Viti Maalum-CHADEMA katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.

Dkt. Macha alifariki dunia Machi 31, 2017 katika Hospitali ya New Cross nchini Uingereza alikokuwa akitibiwa.

Macha aliyekuwa mlemavu wa macho tangu akiwa mtoto wa miezi mitano, amefariki akiwa na umri wa miaka 55 (1962-2017).

Baada ya kuaga mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda nyumbani kwake Moshi mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi.

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Be the first to comment on "TAZAMA LIVE: Mwili wa Mbunge Macha wa Chadema Waagwa Bungeni – Dodoma"

Leave a comment