Tambua Dalili za TB ya Tezi (SCROFULA)

KIFUA kikuu (TB) kinachoathiri tezi au ngozi kitaalamu huitwa Scrofula . Ugonjwa huu husababishwa na vijidudu vinavyosababisha ugonjwa wa kifua kikuu. Vijidudu hivi vikimuingia mtu huweza kuifanya ngozi kuvimba au uso kuvimba au mabakamabaka na  vidonda visivyopona. 

Mara nyingi vijidudu hivyo vikijikita katika vidonda husababisha mtu au mgonjwa kuwa na donda ndugu.

DALILI ZAKE.

Kwa kawaida TB ya ngozi hukua taratibu na kudumu kwa muda mrefu sana mwilini. Vijidudu hivyo ndivyo husababisha kuambukiza tezi hasa zile zilizopo shingoni au sehemu za mabegani. Na baadaye tezi hizo huvimba na hupasuka kisha kutoa usaha na husababisha maumivu makali sana.

Baada ya kupasuka na kutoa usaha, baadaye hufunga lakini siku chache zijazo hupasuka tena. Dalili kubwa ya TB hii ya tezi ni kwamba mara nyingi vidonda vyake vya tezi haviumi.

TIBA YAKE

Ikiwa mgonjwa atagundua ana donda ndugu, uvimbe wa tezi shingoni au kwenye mabega au sehemu nyingine ya mwili, inawezekana kabisa kuwa ana TB aina hii yaani ya tezi. Mgonjwa huyo anashauriwa kwenda hospitali kuonana na daktari ili akamfanyie uchunguzi wa kitaalam kwani TB ya tezi matibabu yake ni sawa na TB nyingine hasa ile maarufu inayojulikana kama kifua kikuu.

Ni vema mgonjwa anapogundulika kuwa na ugonjwa huu, kutumia dawa kama daktari atakavyoelekeza bila kukatiza dozi kwa kuwa tiba yake ni ya muda mrefu.

UGONJWA WA ERYSIPELAS

Ugonjwa huu tumeamua kuuzungumzia kwa kuwa hufanana sana na TB ya tezi, kwani mgonjwa wa Erysipelas huvimba ngozi na kuifanya kuwa na rangi nyekundu. Tofauti na TB ya tezi, uvimbe wa ugonjwa  huu huuma sana na kuleta joto sana mwilini na  uvimbe wake huwa wa kiungo maalum.

Dalili kubwa ya uvimbe wa ugonjwa huu ni kwamba hutawanyika haraka mwilini na kuuma. Ugonjwa huu pia husababisha kuvimba tezi lakini tofauti yake na TB ya tezi uvimbe wake hauumi, hili ni jambo muhimu kulizingatia.

TIBA YAKE

Tiba ya Erysipelas ni tofauti sana na TB ya tezi. Mtu ambaye ameathirika na ugonjwa huu hutibiwa kwa vidonge vya Penicillini kwa kipimo ambacho daktari ataona kinafaa. Iwapo daktari ataona ugonjwa huu umeenea sana mwilini, atamdunga mgonjwa sindano aina ya Procaine Petrinicilline kwa kipimo atakachoona kinafaa. Mgonjwa pia anatakiwa apewe dawa ya kutuliza maumivu kama vile aspirini.

DONDA NDUGU

TB ya tezi pia huweza kusababisha donda ndugu kama tulivyoeleza hapo juu. Mara nyingi vidonda aina hii husababishwa na mzunguko wa damu mwilini. Dalili kubwa ya ugonjwa huu ni kwamba ngozi inayozunguka vidonda huwa nyeusi sana au wanaopata ugonjwa huu ni wale ambao wanapata uvimbe wa mishipa ya damu, kitaalamu huitwa Varicose veins .

Tiba yake kama ni TB, daktari atampa matibabu kama ya kifua kikuu. Vidonda vitatibiwa na viwe vikikandwa kwa maji ya moto. Baada ya kupasuka na kutoa usaha, baadaye hufunga lakini…

USHAURI

Mtu yeyote akiona dalili hizi aende hospitali na kumwona daktari ambapo atafanyiwa vipimo. Ikumbukwe utabibu wa donda ndugu, uponyaji wake huwa taratibu. Ili kuepuka donda ndugu, uvimbe wa mishipa itibiwe mapema, hivyo basi kama utaona dalili zozote tulizozitaja hapo juu, wahi kwenda kumuona daktari kama nilivyoshauri hapo juu ili akufanyie vipimo kisha akigundua kuwa una maradhi haya, atakupa dawa sahihi na bila shaka yoyote utapona.

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment