The House of Favourite Newspapers

Tbl yatangaza Michuano ya soka ya Castle Lager Africa 5s

Dar es Salaam April 24, 2019: Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia Bia yake ya Castle Lager,leo imetangaza rasmi mashindano ya Soka ya  Wanaume  ya Castle Africa 5 – Aside yatakayofanyika Aprili 27,2019 katika Viwanja vyaPosta Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja wa Bia ya Castle Lager Pamela Kikuli, alisema kuwa, fainali za mashindano hayo zitashirikisha timu 32 kutoka kwenye vitongoji mbali mbali vya jijini Dar es Salaam.

Timu hizo ni;

  • Four Ways Park – Kinondoni
  • Terminal Villa – Mbezi mwisho
  • STK Pub – Tabata
  • Namanga Park – Tegeta
  • Jacks Pub – Makumbusho
  • KB Bar – Tegeta
  • Honey Pot – Sinza
  • Mivumoni Resort – Tegeta
  • Maduka matatu – Mwananyamala
  • Kisuma Bar – Mbagala
  • Korner Bar – Sinza
  • Maseo Bar – Mkwajuni
  • Mikumi Bar – Mbagala
  • Mikasa Bar – Ubungo
  • Pade Mapambano – Buza
  • Masai Club – Kinondoni
  • Jambo Lee – Kawe
  • News Sinza Uzuri – Sinza
  • Valabendah – Pugu
  • Ukonga Recreation –Ukonga
  • Texas Bar – Goba
  • Anex Bar – Salasala
  • Benny Pub – Buguruni
  • Shirima Bar – Ubungo
  • Safari Pub – Gongo la Mboto
  • Doctor’s Park – Kibamba
  • Sonata Pub – Chanika
  • Uhuru Park – Buguruni
  • Kilwa Road Bar – Ktemeke
  • Soccer City – Sinza
  • Meeda Bar – Sinza
  • Panama Bar – Kibamba
  • Rungwe Bar – Tabata
  • Pentagoni Bar – Kitunda
  • Green Palm – Kunduchi

Alisema, mashindano hayo ambayo yanafanyika hapa nchini kwa mara ya pili yamekuwa yakifanyika katika nchi nyingine za Afrika ambapo, mwaka jana Tanzania ilishiriki katika mashindano hayo katika kiwango cha kimataifa nchini Zambia kwa upande wa Wanaume.

“Mwaka jana tuliyafanya kwa mara ya kwanza na kupata mwakilishi aliyeshiriki katika michuano ya Kimataifa ya Afrika, huko Zambia kwa kuzikutanisha timu za Afrika ya Kusini, Zimbabwe, Swaziland Lesotho na wenyeji Zambia.

Mashindano Castle Africa 5s ya mwaka huu Tanzania tutakuwa wenyejiambapo yanatarajiwa kufanyika Juni 8,2019.

“Lengo ni kuwafikia wanywaji wa bia ya Castle Lager ikiwa ni pamoja na  kuwapa fursa ya kutimiza ndoto zao,” alisisitiza.

Kikuli pia alisema fainali hizi zitasindikizwa na burudani ya muziki kutoka kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya ambao ni Mr.Blue na Mauwa Sama lakini pia patakuwa na Dj Kwame sambamba na mpiga drum wake.

Nae Meneja Udhamini wa Tbl, David Tarimo alizitaja zawadi za washindi kuwa ni;

TIMU KIKOMBE MEDALI PESA TASLIMU
Bingwa 1 Medali za dhahabu 1,500,000/=
Mshindi wa Pili   Medali za shaba 900,000/=
Mshindi wa tatu   Medali za fedha 600,000/=

Balozi wa Bia ya Castle Lager, Ivo Mapunda aliishukuru Kampuni ya Bia Nchini(TBL) kupitia bia ya Castle Lager kwa  kuwashirikisha Wanawake mwaka huu kwani kwa kufanya hivyo mashindano yam waka huu yatakuwa na msisimuko wa hali ya juu na kuwaomba wakazi wa jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi Viwanja vya Leaders kushuhudia fainali hizo.

Comments are closed.