Castle Lite Extra Cold Draught Yazinduliwa Kwa Shangwe Kubwa Dar

 Kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) kupitia bia yao ya Castle LITE siku ya Jumamosi tarehe 24 Februari walizindua mabomba mapya yanayojulikana kama “Extra Cold Draught Taps” yanayofanya bia yako ya Castle LITE kuwa na ubaridi wa kipekee. Uzinduzi huu ulifanyika Club Elements Masaki jijini Dar es salaam.

 

Akizungumza katika uzinduzi huo Bw. Isaria Kilewo Meneja Masoko Msaidizi wa bia ya Castle LITE amesema “Castle lite imezindua mabomba mapya ambayo yana barafu ili bia inapopita inapata ule ubaridi haswa ili  kumpa mnywaji ladha ya kipekee. Aliendelea kusema kuwa mabomba hayo yamezinduliwa Dar es Salaam ila kutakuwa na maeneo mengine ambayo mabomba haya yatapatikana.

Meneja Masoko wa bia ya Castle LITE Bi. Amou Majok na Meneja Masoko Msaidizi Bw. Isaria Kilewo walikionesha gloves zao tayari kwa kuzindua Extra ColdDraught Taps katika uzinduzi uliofanyika Club Elements

Matukio mengine katika picha

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment