TECNO NA TIGO WATAMBULISHA RASMI PHANTOM 9
Kampuni maarufu ya simu nchini TECNO ikishirikiana na TIGO imezindua rasmi simu yao kubwa ya TECNO Phantom 9 ikiwa ni mwendelezo katika matoleo ya Phantom ikiambatanishwa na ofa ya GB 18. TECNO Phantom 9 ni simu ya kwanza katika upande wa TECNO Phantom series kuja na kamera tatu za teknolojia ya AI (AI triple) zenye 16MP+8MP+2MP. Akizungumza na mbele ya waandishi wa habari, Meneja wa Uhusiano wa Kampuni ya TECNO, Bwana Eric Mkomoye alisema kwamba;
“Katika ulimwengu wa sasa wa smartphone, kamera zinapata ushindani mkubwa toka kwa kamera za simu kwani kila mpiga picha anatambua umuhimu wa kutumia simu yenye kupiga picha vizuri ili kuepuka usumbufu wa kujibebesha mizigo na TECNO tumelifanyia kazi kupitia Phantom 9 kwani ina kila sifa zenye kukidhi haja ya wateja wetu wanaopenda kuchukua matukio kupitia kamera za simu zao.
“TECNO Phantom 9 ikiwa kama ‘flag ship’ ya kampuni kwa mwaka huu, Tecno imehakikisha ujuzi si katika upande wa kamera tu bali hata uwezo wa kuhifadhi files na speed ni mkubwa ikipewa uwezo na memory yenye GB 128Rom + 6Ram pamoja na Operating system ya Android Pie (P). Vilevile Phantom 9 ina AMOLED Screen ya nch 6.4 FHD yenye kupiga picha zenye rangi halisi na upana zaidi,” alisema Mkomoye.
Meneja Mawasiliano wa TIGO Tanzania, Bi. Woinde Shisael alizungumza machache kuhusiana na ushirika uliopo baina ya kampuni hizo mbili na namna ambavyo wateja wa Tigo watakaonunua simu hii ya Phantom 9 katika maduka ya Tigo au katika maduka ya wabia wa Tecno watakanufaika na ofa ya mpaka GB 96 kutoka TIGO.
“TECNO na TIGO tukiwa kampuni pendwa na zenye kujali wateja wetu tunafahamu ni kwa namna gani wateja wetu wanatamani kwenda sambamba na mfumo wa maisha ya kidigitali na kwa kuzingatia hilo tumeileta rasmi Phantom 9 ikiwa na ofa ya mpaka GB 98 kwa mwaka mzima ili wateja wetu waendelee kufurahia mtandao bora wakiperuzi mitandaoni.”
Wateja wote wanaotaka kununua Phantom 9 wanaweza kuweka oda za awali (pre-order) katika maduka ya TECNO smart hubs yaliyoko Dar es salaam, Mtaa wa Samora, Kariakoo katika Jengo la China Plaza na pia Mlimani City, kwa kiasi cha shilingi 50,000 kitapokelewa na siku ya kuja kuchukua simu mteja atamalizia pamoja na kupewa zawadi maalum.
Imeandaliwa na Neema Adrian/GPL
Comments are closed.