The House of Favourite Newspapers

Tecno Wamezindua Phantom 6 na Phantom 6 Plus

Kampuni inayoongoza kwa mauzo ya simu Afrika, Tecno Mobile imezindua simu mbili matata za Phantom 6 na Phantom 6 Plus katika tukio lililohudhuriwa na watu maarufu kibao katika Hotel ya Armani ambayo ipo katika jengo refu zaidi duniani “Burj Khalifa”. Uzinduzi huu umefanyika wakati ambapo kampuni ya Tecno inatimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake.

ANGALIA KIPANDE KIFUPI CHA VIDEO YA TECNO PHANTOM 6

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi Naibu amesema “Imetuchukua takribani miaka 3 katika matengenezo yake na imehusisha zaidi ya wahandisi laki 5” amesema Mkuu wa Masoko wa Tecno, Vane Ni

“TECNO Phantom 6 inawapa watumiaji wa simu za mkononi utulivu bora pindi wanapotumia, kasi na kamera bora na nzuri ili kufurahia zaidi simu ya mkononi” amesema Naibu Kiongozi wa Masoko wa Tecno Nigeria, Attai Oguche.

Uzinduzi ulifana sana ambapo kulikuwa na zaidi ya vyombo vya habari 70 tofauti kutoka chini mbalimbali duniani kote na miongoni mwa mastaa waliohudhuria ni mwanamuziki mahiri wa Tanzania, Ali Kiba na mwanahabari “Mtu wa Nguvu Millard Ayo ambaye alishinda safari ya kwenda China.

Mwanahabari wa Tanzania Millard Ayo akitangazwa mshindi wa Safari Safari ya China.

Mwanamuziki wa kimataifa wa Tanzania, Ali Kiba akiwa na kifaa kipya cha Phantom 6 akifanya mauzungumzo.

Baada ya uzinduzi huo Tecno Tanzania ikatangaza kwamba Phantom 6 na Phantom 6+ zitaanza kupatikana rasmi kuanzia tarehe 8 Oktoba 2016 katika duka la Tecno lililopo City Mall Posta ambapo wateja wote watakaonunua Phantom 6 siku hiyo watapatiwa vifurushi vya zawadi na kutakuwa na zawadi kubwa nono.

Pia wakatangaza kwamba kuanzia Jumatatu tarehe 3 Oktoba wateja watajaza fomu maalum ili kuweka oda zao na watazawadiwa zawadi mbalimbali zikiwemo T-Shirts, mabegi, T-Band na Sefie stick siku ya kuanza mauzo hiyo tarehe 8 Oktoba. Kuhusu bei kwakweli Tecno wameangalia hali halisi ya uchumi kwa sasa ambapo gharama itakuwa kati ya Tsh 500,000 – Tsh 600,000.

TOFAUTI KATI YA PHANTOM 6 NA PHANTOM 6+


Kwa taarifa zaidi unaweza kutembelea kurasa za mitandao ya kijamii ya Tecno na hakikisha hukosi mojawapo ya simu hizi kali ambazo zimekuja kufanya mageuzi ya teknolojia.

Facebook: https://www.facebook.com/TECNOMobileTanzania/?fref=ts

Instagram: https://www.instagram.com/tecnomobiletanzania/

Twitter: https://twitter.com/TECNOMobileTZ

Comments are closed.