visa

TECNO YAJA NA MOTO WA PHANTOM 9

Hatimaye baada ya kimya kirefu, TECNO Mobile Tanzania yaileta Phantom 9. Huu ukiwa muendelezo wa simu za Phantom zilizoanza kutolewa takribani miaka 4 iliyopita.

 

 

Tukio rasmi la uzinduzi lilifanyika katika duka bora kabisa (Smarthub) la Mlimani City likihudhuriwa na wapenzi wa TECNO, wasanii na vyombo vya habari.

TECNO iliweza kumtambulisha rasmi balozi wa Phantom 9, ambaye ni muigizaji nguli, ndugu Gabo Zigamba. Katika uzinduzi huo pia ilishuhudiwa kampuni ya simu, TIGO ikileta ofa ya GB 98 kwa miezi sita ili wateja wao waendelee kufurahia mtandao bora wakiperuzi mitandaoni.

 

Kipi hasa kinasifika katika simu mpya ya Phantom 9? Moja ya vitu vya kipekee zaidi ni aina tatu za kamera ya mbele za mbele zilitongenezwa katika mfumo wa akili bandia (Artificial Intelligence). Zina uwezo wa 16MP+8MP+2MP.
Vilevile, uwezo wa kuhifadhi files na speed ikiwa imepewa uwezo wa memory yenye GB 128 ROM na 6 GB RAM pamoja na Operating system ya Android Pie (P). Vilevile inakuja na kioo cha AMOLED chenye screen ya nchi 6.4 FHD.

 

Muundo wa simu hii ni ya kipekee kabisa. Ikiwa na rangi ya Aurora, mfumo wa ulinzi pia umekuja na ‘in display fingerprint’, ikimaanisha uwezo wa kubonyeza juu ya kioo kufungua simu yako. Uwezo wa betri ni 3500mAh. Inakuja pia teknolojia ya 4G.

 

Phantom 9 imekuja muda ambao kampuni ya TECNO imezindua upya mwezi Julai kauli yao inayoitwa, ‘Expect More’ badala ya Experience More. Hii ikimaanisha wateja watarajie mambo makali zaidi. Uzinduzi huu umeambatana na kusainishwa mkataba mpya baina ya TECNO na timu ya soka nchin uingereza, Manchester City.
TECNO Mobile wamedhamiria kuhakikisha moto unaendelea kuwaka katika mapinduzi ya teknolojia ya simu. Na mwezi huu wameanza na Phantom 9. Kwa hakika, tuendelee kutarajia zaidi kutoka kwao.
Toa comment