The House of Favourite Newspapers

Uchaguzi Marekani, Ted Cruz Ambuluza Trump

0

ted-cruz-wants-you-to-think-hes-extremely-conservativeSeneta wa Texas Ted Cruz.

IOWA, MAREKANI

Seneta wa Texas Ted Cruz ameshinda mchujo wa mgombea wa uchaguzi kupitia Chama cha Republican katika jimbo la Iowa, Marekani. Huo ndio mchujo wa kwanza katika uchaguzi wa urais wa 2016 ambao utafanyika baadaye mwezi Novemba. Cruz amepata asilimia 28 ya kura.
donald-trump-wants-to-wage-economic-war-on-mexico-to-get-them-to-pay-for-a-border-wall

Donald Trump

“Huu ni ushindi wa wahafidhina jasiri,” mgombea huyo amesema baada ya kubainika kwa ushindi wake. Mfanyabiashara Donald Trump alikuwa akiongoza kwenye kura za maoni kabla ya kura kupigwa lakini sasa amekuwa wa pili akipata asilimia 24 ya kura zilizohesabiwa.

Seneta wa Florida Marco Rubio amefanya vyema kuliko ilivyotarajiwa amekuwa wa tatu akipata akipata asilimia 23 ya kura zilizohesabiwa.

Kura za mchujo wa chama cha Democratic bado zinahesabiwa.
Asilimia 85 ya kura ambazo zimehesabiwa zinaonyesha pengo kati ya Hillary Clinton na mshoshialisti wa Chama cha Democratic, Bernie Sanders ni 1% pekee.

Akizungumza baada ya matokeo kujulikana, Marco Rubio amempongeza Bw Cruz na kusema ndiye mgombea ambaye anaweza kuunganisha chama cha Republican ambacho kimegawanyika.

Dakika chache baadaye, Bw Trump alipanda jukwaani katika ukumbi mwingine na kumpongeza seneta huyo wa Texas, na kusema anaridhika kumaliza katika nambari mbili.
Wagombea wawili wamejiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho.

Upande wa Republican, gavana wa zamani wa Arkansas Mike Huckabee ameandika kwenye Twitter kwamba atasitisha kampeni yake.

Matokeo ya Iowa

Chama cha Republican, 99% ya kura:

  • Ted Cruz: 28%, wajumbe wanane
  • Donald Trump: 24%, wajumbe saba
  • Marco Rubio: 23%, wajumbe saba
  • Ben Carson: 9%, wajumbe watatu

Chama cha Democratic, 99% ya kura:

  • Hillary Clinton: 50%, wajumbe 22
  • Bernie Sanders 50%, wajumbe 21

Asilimia 85 ya kura ambazo zimehesabiwa zinaonyesha pengo kati ya Hillary Clinton na mshoshialisti wa chama cha Democratic Bernie Sanders ni 1% pekee.

Leave A Reply