The House of Favourite Newspapers

Tekno Afuata Nyendo Za Diamond, Davido Na Wizkid

 

MSANII Augustine Miles Kelechi maarufu kama Tekno Miles toka Nigeria, amefuata nyendo za wasanii wenzake waliomtangulia kwenye muziki baada ya kufungua lebo yake mpya ya ‘Cartel Records’.

 

Meneja wa msanii huyo, ‘John Peace’ amethibitisha taarifa hizo katika mtandao wa burudani nchini  Nigeria kwamba Tekno ameondoka katika lebo yake ya awali  ya Triple MG na kuelekea kwenye lebo yake aliyofungua ya Cartel Records.

 

Msanii huyo pia amejitambulisha kuwa yeye ni mmiliki kamili wa lebo hiyo kwenye akaunti yake ya instagram kwa kuweka picha yenye jina la lebo yake ikiwa na maelezo yanayosomeka ‘CEO’.

 

 

Baadhi ya wasanii wengine wanaomiliki lebo  za muziki  Diamond Platnumz (WCB), Davido (DMW), Patoranking (Amari Musiq) Wizkid (Starboy Music Entertainment).

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.