The House of Favourite Newspapers

Televisheni za Kenya Zasimamisha Kuonesha Matokeo ya Awali ya Kura ya Urais

0

 

VYOMBO vya habari vya Kenya vimesimamisha kutangaza matokeo ya awali ya kura ya urais nchini humo, na hivyo kuzusha maswali kuhusu matokeo hayo katika kipinbdi hiki ambacho mchakato wa kuhesabu kura ukiingia siku yake ya nne.

 

Mashirika ya utangazaji hayajatoa maelezo yoyote kuhusu kusitishwa wa ghafla kwa zoezi hilo, jambo ambalo lilikuwa lifanyika na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi IEBC Wafula Chebukati akiwatoa wakenya wasiwasi kuhusu kile kilichoonekana kama matokeo tofauti yanayoratibiwa na vituo mbalimbali vya televisheni.

 

Kwa sehemu kubwa uchaguzi wa huu wa Jumanne umekuwa wa amani, tofauti na chaguzi za miaka ya nyuma ambazo ziligubikwa na visa vya ghasia, ambavyo wakati mwingine vilihusisha matukio ya umwagaji wa damu. Mchuano mkali katika uchaguzi huu wa sasa ni kati ya William Ruto and Raila Odinga.

BUMBULI NAE OUT YANGA! WATANGAZA RASMI KUACHANA NAE, NI WIKI 2 TU TANGU SENZO AONDOKE…


 

Leave A Reply