The House of Favourite Newspapers

Tembo Afariki Kwa Kutembea Zaidi ya Km 1,700

0

Tranquillised-wild-elephant TEMBO mmoja aliyetenganishwa na wenzake kwa zaidi ya miezi miwili kutokana na mafuriko, alijikuta akitembea zaidi ya kilometa 1,700 kati ya India na Bangladesh kabla ya kufa jana kutokana na uchovu na ukosefu wa chakula.

Mnyama huyo ambaye aligunduliwa na wataalam wa wanyama mwishoni mwa mwezi Juni akiwa amechoka, alipatiwa huduma ya madawa mara tatu huku pakifanywa mpango wa kumsafirisha kumpeleka katika mbuga ya wanyama ya Bangladesh.

Tranquillised-wild-elephantw“Mnyama huyo alifariki jana,” alisema ofisa wa wanyamapori, Ashit Ranjan Paul akizungumza na shirika la habari la AFP.

“Tumefanya kila juhudi kumwokoa mnyama huyo ambapo maofisa zaidi ya kumi wakiwemo walinzi wa wanyamapori, matabibu wa wanyama na polisi, tulimfuatilia na kumhudumia kwa juhudi zote katika saa zake 48 za mwisho.  Hata hivyo, ilikuwa ni bahati mbaya,” aliendelea kusema.

Paul alisema aliamini mnyama huyo alitokea kaskazini-mashariki mwa Jimbo la Assam nchini India, lakini alipofika Bangladesh alicharuka na kukimbilia katika bwawa ambako wanakijiji wa sehemu hiyo walimwokoa mnyama huyo mwenye uzito wa tani nne, asizame.

Vyombo vya habari vya sehemu hiyo vililaumu matibabu kwamba walimdunga mnyama huyo dawa nyingi kupita kiasi za kutia usingizi ambazo zilimfanya awe mnyonge zaidi.

Leave A Reply