The House of Favourite Newspapers

TESSY AFUNGUKIA KUPIGWA NA CHUCHU

Tessy Chocolate

MZAZI mwenzake na msanii wa Bongo Fleva, Aslay Isihaka, Tessy Chocolate amefunguka kwamba katika maisha yake hakuna mtu amewahi kumpiga zaidi ya mama yake mzazi, hivyo tetesi zinazosambaa mitandaoni kuwa amepigwa na msanii wa Bongo Movie, Chuchu Hans siyo za kweli.  Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Tessy alisema kwamba, anashangaa watu wanavyosema kuwa hivi karibuni alikutana na kichapo toka kwa Chuchu baada ya kudaiwa kumfumania na mzazi mwenzake, Vincent Kigosi ‘Ray’ wakiwa kwenye gari jambo ambalo si kweli.

“Uuwii jamani mimi mara yangu ya mwisho kupigwa ilikuwa ni miaka kadhaa iliyopita tena nilipigwa na mama yangu mzazi, tokea hapo hakuna mtu mwingine aliyewahi kuugusa mwili wangu kwa kunipiga, sasa nashangaa ninavyosikia kwamba eti hivi karibuni nilipigwa na Chuchu, sio kweli jamani sio kweli kabisa,” alisema Tessy

MSIKIE RAY

Hata hivyo, Risasi Mchanganyiko lilifanikiwa kuongea na Ray pia ambaye naye alishtushwa na habari hizo nakusema kwamba watu wanaongea vitu ambavyo hawana uhakika navyo.

“Jamani nani kawaletea hizo habari? Kwa sababu nina kama wiki moja tangu nirudi toka Afrika Kusini ambako nilienda kuandaa filamu, sasa hiyo ishu ilitokea lini wakati mimi sikuwa hapa nchini? Unajua nashangaa sana kuambiwa hayo mambo, huyo aliyewaletea hizo taarifa kawaongopea mimi najiheshimu sana na siwezi kufanya mambo kama hayo,” alisema Ray.

Gazeti hili halikuishia hapo kwani lilifanya jitihada za kumtafuta Chuchu, ambapo baada ya kupatikana hakutaka kuongea sana zaidi ya kusema tu hayupo tayari kuongelea ishu hizo. “Sipo tayari kuongelea hizo habari,” alisema Chuchu kwa kifupi na kukata simu.

Stori: Memorise Richard, RISASI MCHANGANYIKO

Comments are closed.