TESSY AFUNGUKIA MADAI YA KUVALIANA NGUO NA UWOYA

BAADA ya picha yake kusambaa mitandaoni akiwa amevaa nguo sare na aliyowahi kuonekana ameivaa msanii wa filamu za Kibongo, Irene Uwoya na mashabiki kuanza kum-simanga kwamba ame-iazima, mrembo Tessy Abdul ‘Tessy Chokolate amefungukia madai hayo. Akipiga stori na Ijumaa Wikienda Tessy ambaye ni mzazi mwenzake na msanii wa Bongo Fleva, Aslay Isihaka, alisema ameshangaa jinsi watu walivyo-msema vibaya huko mitandaoni kwamba ameazima gauni kwa Uwoya wakati siyo kweli.

“Mimi siwezi kuvaliana nguo na mtu yoyote yule, kwa nini nifanye hivyo? Lile gauni nililovaa nililinunua mwenyewe dukani kwa pesa zangu, naomba waniache jamani, hebu wafuatilie vitu vya maana kutoka kwangu, wanisapoti hata kwenye hii saluni yangu niliyofungua nitawashukuru sana ila sio kufuatilia mambo ya kizushi,”alisema

STORI: MEMORISE RICHARD

Toa comment