The House of Favourite Newspapers

Tessy: Kwa Aslay Kama Ipoipo tu!

Tessy Chocolate

MZAZI mwenzake staa wa Bongo Fleva, Aslay Isihaka ‘Dogo Aslay’, Tessy Chocolate amefunguka kuwa kama imepagwa aoane na msanii huyo itakuwa tu licha ya kuwa kwa sasa wamemwagana.

Tessy alitoa kauli hiyo hivi karibuni alipoulizwa kuhusu hatma ya penzi lake na Aslay baada ya mwanahabari wetu kuona wamehudhuria futari iliyoandaliwa na muigizaji Irene Uwoya huku kila mmoja akiwa na hamsini zake.

“Tumetengana ndio lakini kama ipo ipo tu, kama amepangwa awe mume wangu atakuwa tu,” alisema Tessy. Aslay alipoulizwa kuhusu ishu hiyo hakutaka kuzungumza lolote.

Stori: Imelda Mtema

Comments are closed.