The House of Favourite Newspapers

Tetekuwanga kwa watoto

teteTetekuwanga ni miongoni mwa magonjwa yanayowasumbua watu wengi, hususan watoto. Ugonjwa huu husababishwa na Virusi vya Varicel Zoster na huambukizwa kwa haraka sana. Mgonjwa wa tetekuwanga, hutokwa na vipele vingi mwili mzima, vinavyofanana na malengelenge ambavyo huwasha sana.

Watoto wachanga hushambuliwa zaidi na ugonjwa huu kwa sababu kinga ya miili yao inakuwa bado haijakomaa na utafiti usio rasmi, unaeleza kwamba kila mtu hupata ugonjwa huu angalau mara moja katika maisha yake, kwamba kama hukuupata utotoni, basi utaupata hata ukiwa mtu mzima.

DALILI ZA TETEKUWANGA

Dalili za awali za tetekuwanga, huwa ni kupatwa na homa kali ambayo baadaye hufuatiwa na vipele ambavyo huanzia mwilini na kusambaa mpaka usoni na kichwani. Vipele hivi huwasha sana na vikipasuka, hutoa majimaji au usaha na kuacha kovu ambalo hufutika taratibu sana. Hata hivyo, makaovu mengi ya tetekuwanga hufifia taratibu na baadaye kufutika kabisa.

Dalili nyingine za ugonjwa huu ni mwili kuishiwa nguvu Fatigue, kukosa hamu ya kula na maumivu makali ya kichwa.

Ugonjwa huu huambukizwa kwa urahisi kutoka kwa mgonjwa mmoja kwenda kwa mwingine kwa kugusana au kwa njia ya hewa. Ni rahisi kwa mtoto mwenye tetekuwanga kuwaambukiza wenzake wengi anaocheza nao.

Chanjo ya tetekuwanga kwa watoto, huweza kuwakinga dhidi ya ugonjwa huu.

Kwa kawaida, hakuna tiba ya moja kwa moja ya tetekuwanga, upo ushahidi wa wagonjwa wengi ambao walipona bila hata kutumia dawa yoyote ingawa kumuona daktari haraka mara baada ya kuanza kuona dalili za awali, hupunguza madhara ya ugonjwa huo. Ukiona mwanao ana dalili za tetekuwanga, muwahishe hospitali.

Comments are closed.