The House of Favourite Newspapers

Tetemeko la ardhi laua 77 Ecuador

1

2

Baadhi ya maeneo yaliyoharibiwa na tetemeko.

TAKRIBANI watu 77 wamepoteza maisha huku zaidi ya 500 wakijeruhiwa baada ya tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa ritcher 7.8 kuikumba Ecuador usiku wa kuamkia leo.  Makamu wa Rais wa nchi hiyo, Jorge Glas amethibitisha.

Tetemeko hilo kubwa kuwahi kutokea Ecuador tangu mwaka 1979, limetokea jirani na Mji wa Muisne.

1

Baadhi ya majeruhi wa tetemeko hilo.

Miongoni mwa madhara ya tetemeko hilo ni pamoja na kuharibu miundombinu ikiwemo madaraja, barabara na hospitali.

Rais wa nchi hiyo, Rafael Correa, ambaye ameamua kukatiza ziara yake ya Italia na kurejea nyumbani ametangaza hali ya hatari.

Katika hotuba yake aliyoitoa baada ya taarifa za tetemeko hilo, rais huyo amesema; “Hili ni pigo linaloumiza. Nawaomba wananchi kuwa watulivu na kushikamana. Tuwe na nguvu; hili janga tutalikabili”

Aliongeza kuwa: “Barabara na hospitali vinaweza kujengwa upya; lakini uhai wa watu hauwezi kurudishwa na hilo ndilo linalosikitisha zaidi.”

1 Comment
  1. […] Baadhi ya majeruhi wa tetemeko hilo. Miongoni mwa madhara ya tetemeko hilo ni pamoja na kuharibu miundombinu ikiwemo madaraja, barabara na hospitali. Rais wa nchi hiyo, Rafael Correa, ambaye ameamua kukatiza ziara yake ya Italia na kurejea nyumbani ametangaza hali ya hatari. Katika hotuba yake aliyoitoa baada ya taarifa za tetemeko hilo, rais huyo amesema; “Hili ni pigo linaloumiza. Nawaomba wananchi kuwa watulivu na kushikamana. Tuwe na nguvu; hili janga tutalikabili” Aliongeza kuwa: “Barabara na hospitali vinaweza kujengwa upya; lakini uhai wa watu hauwezi kurudishwa na hilo ndilo linalosikitisha zaidi.” Article Source: Tetemeko la ardhi laua 77 Ecuador […]

Leave A Reply