The House of Favourite Newspapers

Tetemeko la Ardhi Laua Watu 13 Pakistan na Afghanistan, 100 Wapelekwa Hospitalini

0

Tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 6.5 kwenye vipimo vya rikta limetikisa sehemu kubwa ya Pakistan na Afghanistan Usiku wa kuamkia leo na kupelekea wakazi waliokumbwa na wasiwasi kuondoka kwenye nyumba zao pamoja na ofisi.

Hofu pia ilitanda kwenye maeneo ya vijiji, wakati watu 13 wamekufa kutokana na tukio hilo. Zaidi ya watu 100 walipelekwa hospitalini kutokana mshtuko kwenye bonde la Swat, lililopo kwenye jimbo la kaskazini magharibi mwa Pakistan la Khyber, kulingana na Bilal Faizi ambaye ni msemaji wa huduma za dharura za taifa hilo, akizungumza na shirika la habari la AP.

Taimoor Khan ambaye ni msemaji wa timu ya dharura ya jimbo hilo amesema kwamba nyumba kadhaa zilizotengenezwa kwa matofari ya udongo ziliporomoka kweye maeneo ya vijijini. Tetemeko hilo pia linasemekana kusababisha watu wengi kuondoka nyumba zao pamoja na ofisi kwenye mji mkuu wa Pakistan wa Islamabad. Ripoti kutoka kwa vyombo vya habari zinasema kwamba baadhi ya nyumba za makazi mjini humo zilipata nyufa.

Leave A Reply