The House of Favourite Newspapers

TFF: Fei Toto Bado ni Mchezaji wa Yanga kwa Mujibu wa Mkataba

0

 

                                 Kiungo wa Klabu ya Yanga Feisal Salum ‘Fei Toto’

 

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imeamua kuwa Feisal Salum (Fei Toto) bado ni mchezaji wa Yanga kwa mujibu wa mkataba.

Katika taarifa yake iliyotolewa leo, Januari 7, 2023 na kusainiwa na Cliford Ndimbo, Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, uamuzi kamili wa pande zote mbili zilizokuwa zinahusika kwenye shauri hilo, utatolewa Jumatatu, Januari 9, 2023.

Kamati ya Sheria na hadhi za Wachezaji ilisikiliza malalamiko hayo jana ambapo pande zote  (Yanga na Feisal Salum) ziliwakilishwa na wanasheria wao

Yanga ilikuwa na  mgogoro wa kimkataba ambapo kiungo huyo inaelezwa alivunja mkataba wake na Yanga ili kuwa huru kujiunga na timu nyingine, huku Yanga ikidai bado ina mkataba naye.


Leave A Reply