Kartra

TFF: Mechi ni Kule Kule Kigoma

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limetoa taarifa kuwa hakuna mabadiliko ya uwanja ambao utapigiwa fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), kati ya Yanga dhidi ya Simba, Julai 25 mwaka huu.

 

Watani hao wa jadi wanatarajia kumenyana kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma ambapo hivi karibuni ziliibuka tetesi zikidai kwamba huenda uwanja ukabadilishwa kutokana na ukubwa wa mchezo huo.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo, alisema: “Hizo ni tetesi tu za kubadilishwa kwa uwanja, mchezo utapigwa hapohapo kama ilivyopangwa awali.

 

Kuelekea mchezo huo, Yanga kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Injinia Hersi Said, alisema: “Tumejiandaa vizuri kwa ajili ya kuhakikisha tunaibuka na ushindi dhidi ya Simba katika mchezo wetu wa fainali wa Kombe la Shirikisho. Muhimu katika mchezo huu ni kubeba taji hilo. Tunakwenda kwa ajili ya kushinda na si kingine.”

STORI: LEEN ESSAUDar es Salaam


Toa comment