TFF WAANIKA VIIINGILIO VYA MECHI YA SIMBA NA YANGA

 

Kikosi cha timu ya Simba.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kati ya Simba na Young Africans utakaochezwa Septemba 30, 2018 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

 

Viingilio hivyo ni shilingi 30,000 kwa VIP A, B na C ikiwa 20,000 huku mzunguko itakuwa ni 700 pekee.

 

Mechi inayosuburiwa kwa hamu na wadau pamona na mashabiki wa soka nchini itakuwa ya aina yake kutokana na utaaduni wa timu hizo mbili kujawa na hamasa kubwa pale zinapokutana.

Kikosi cha Yanga.

Katika mchezo wa mwisho uliofanyika Uwanja wa Taifa msimu uliopita, Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na mchezaji kiraka, Erasto Nyoni.

Loading...

Toa comment