TFF Wafunguka Kurejesha Mechi za Ligi Kuu Bara
SHIRIKISHO la soka nchini (TFF), limeweka wazi kuwa linashirikiana na Bodi ya Ligi (TPLB), kuhakikisha ligi kuu inarejea, lakini bado mchakato huo ni wa ndani kwani unategemea tamko la serikali juu ya mwenendo wa janga la Corona.
Taarifa ya TFF jana Mei 5, 2020, imeeleza kuwa mchakato wa ndani kati ya shirikisho na bodi pamoja na wadau ikiwemo vilabu, unaendelea.



