TFF WAKOSA ZAWADI YA SIMBA

LICHA ya Jana klabu ya Simba kukabidhiwa Kombe na medali za ubingwa, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura amesema mpaka sasa hawajajua watapataje fedha za kuwapa
Simba.

Wambura amesema siku zote zawadi za washindi hutolewa na mdhamini mkuu wa ligi lakini kwa bahati mbaya msimu huu hawakuwa na mdhamini hivyo wanalazimika wao kama bodi kutafuta zawadi hizo.

 

Akizungumza na Spoti Xtra Wambura alisema wadhamini wengi ambao walikuwa wanajitokeza hawakukidhi kiwango cha bajeti ambayo walikuwa wanahitaji.

 

”Ligi inamalizika hatujui tutapataje pesa ya kumpa bingwa ambaye ni Simba, kwa sababu siku zote mdhamini mkuu ndiyo huwajibika kutoa zawadi kwa washindi. “Kwa kuwa ligi ya msimu huu tulikosa mdhamini mkuu sisi kama bodi ya ligi tunawajibika kutafuta pesa za kuwapa washindi ambapo hadi hivi sasa bado hatujajua tunazipataje,” alisema Wambura.

 

Katika hatua nyingine, JKT Tanzania imefufua matumaini yake ya kusalia ligi kuu baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo uliopigwa jana asubuhi katika viwanja vya JMK Park, Dar es salaam.

 

Ushindi huo wa Jana wa JKT uliwafanya wafikishe pointi 44 wakipanda nafasi nne na kushika nafasi ya 15 katika msimamo na kuweka hai matumaini ya kutoshuka daraja.Mabao yote ya JKT yalifungwa na Hassan Materema


Loading...

Toa comment