TBC Yasaini Mkataba Wa Bilioni 3 na TFF – Video

Rais wa TFF Wallace Karia (Kulia) na Mratibu wa Miradi na Masoko TBC Gabriel Nderumaki (kushoto) wakisaini Mkataba wa haki za matangazo ya Mpira wa Miguu ya Ligi Kuu wenye thamani ya shilingi Bilioni 3 kwa miaka 10.

Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) limeingia mkataba wa kurusha matangazo ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa miaka 10 wenye thamani ya shilingi Bilioni 3.54. Mkataba huo unaipa TBC pekee haki ya kurusha matangazo kwa sauti, na chombo kingine kikitaka kurusha matangazo kwa sauti lazima kiwe na makubaliano na TBC.

 

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema haki ya urushaji wa matangazo ya mpira wa miguu kwa njia redio ipo kwa TBC, kwa vyombo vingine vya habari haviruhusiwi kurusha matangazo bila kupata kibali kutoka TBC.

 


Toa comment