The House of Favourite Newspapers

TFF Watangaza vita na MUSIBA, Wampa Siku 7 Tu! – Video

Shirikisho la Soka chini TFF limekanusha taarifa zilizochapishwa katika baadhi ya vyombo vya habari kuwa limehusika na matumiza mabaya ya fedha kiasi cha shilingi million 300 kutoka katika vyanzo mbalimbali vya shirikisho hilo.

 

Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya shirikisho hilo yaliyopo karume jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidau amesema habari hizo siyo za kweli na ameyataka magazeti yaliyochapisha kuthibitisha ukweli wa jambo hilo vinginevyo watawachukulia hatua kwa kulichafua shirikisho hilo.

 

Kidau amesema TFF imekata rufaa kupinga maamuzi ya mahakama ya kumrejesha madarakani aliekuwa Makamo wa Rais wa TFF, Charles Wambula aliyeshinda kesi ya kufungiwa maisha kujihusisha na soka na kamati ya maadili ya shirikisho hilo.

 

Pamoja na mambo mengine Kidau pia ametolea ufafanuzi juu ya sakata la fedha za mshindi wa Kombe la Shirikisho maarufu Azam Confederation Cup, shilingi million 50 ambazo vilabu vya Simba na Mtibwa hawajalipwa hadi sasa ambapo amesema TFF wannshirikiana na Azam kuhakikisha fedha hizo zinatolewa kwa wakati.

VIDEO: WASKIE TFF WAKITOA TAMKO

Comments are closed.