The House of Favourite Newspapers

VODACOM WAONDOKA LIGI KUU, KENYA YATOA DOZI CECAFA

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) kupitia Bodi ya Ligi limeweka wazi kuwa ligi kuu msimu ujao itakuwa na wadhamini wawili ambao ni Azam Pay TV na Benki ya KCB baada ya kampuni ya mawasiliano ya Vodacom kumaliza mkataba wake.

 

Kwa mujibu wa barua iliyotumwa na Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura, inasema kuwa ligi hiyo itakuwa na wadhanini hao ambapo Azam watakuwa na haki ya matangazo wakati KCB wakiwa ni wadhamini wenza kwenye ligi hiyo.

Barua hiyo inaeleza kuwa udhamini huo utakuwa na malipo ya kiasi cha sh milioni 162 kutoka Azam Pay TV kwa klabu, wakati malipo kutoka KCB yakiwa ni sh milioni 15.

 

Kufuatia barua hiyo kutoka Bodi ya Ligi Championi Jumatano lilimtafuta rais wa TFF, Wallace Karia ambaye alifunguka kuwa: “Suala la wadhamini litakapokuwa tayari litawekwa wazi kwa sababu tuna utaratibu wa kuwajulisha wadau wetu maana mtachokonoa matokeo yake tukatoa taarifa ambazo zinatuharibia mipango yetu,” alisema Karia.

 

Wakati huohuo, kwenye michuano ya Vijana ya Cecafa chini ya miaka 17 iliyoendelea jana, timu ya vijana ya Kenya ilifanikiwa kuwachapa Sudan ya Kusini mabao 4-0.

 

Comments are closed.