The House of Favourite Newspapers

TFF Yamruhusu Saido Kukiwasha Dhidi ya Dodoma Leo

0

UONGOZI wa Yanga umepokea kibali kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) cha kumruhusu kiugo wao mshambuliaji raia wa Burundi, Said Ntibazonkiza ‘Saido’ cha kumruhusu kucheza mchezo dhidi ya Dodoma Jiji FC.

 

Yanga inatarajiwa kuvaana na Dodoma katika mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kupigwa leo kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.

Kiungo huyo ni kati ya wachezaji wapya waliosajiliwa na timu hiyo katika usajili huu wa dirisha dogo lililofunguliwa Jumatano iliyopita baada ya kukamilisha taratibu zote za usajili wa nyota huyo mpya.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, alisema kuwa tayari kamati yao ya mashindano iliyo chini ya Injinia Hersi Said imefanikisha taratibu za usajili wa Saido kwenye shirikisho hilo.

 

Aliongeza kuwa baada ya uongozi kukamilisha taratibu zote, suala la kucheza au kutocheza limebaki kwa Kocha Mkuu, Mrundi, Cedric Kaze ambaye yeye ndiye mwenye jukumu la kuamua mchezaji yupi wa kumtumia.“

 

Tayari Kamati ya Mashindano ya Yanga imefanikisha usajili wa mshambuliaji wetu Saido raia wa Burundi baada ya kukamilisha taratibu zote za usajili TFF.“

 

Hivyo huenda akawa sehemu ya kikosi kitakachocheza mchezo wetu wa ligi kesho (leo) dhidi ya Dodoma Jiji ambao tunauchukulia umuhimu mkubwa katika kupata pointi tatu ili tuendelee kukaa kileleni katika raundi hii ya kwanza ya ligi.“

 

Hakuna mtu asiyefahamu uwezo wa Saido, ninaamini uwepo wake katika timu ataongeza kitu kwani lipo wazi ana uzoefu mkubwa katika soka na hiyo ni baada ya kucheza Ulaya katika miaka kadhaa iliyopita,” alisema Mwakalebela.

Stori na Wilbert Molandi, Dar es Salaam

Leave A Reply