The House of Favourite Newspapers

TFF yamzuia Yondani kuivaa Azam

Kelvin Yondani

BEKI wa Yanga, Kelvin Yondani amefungiwa mechi tatu baada ya kumpiga ngumi mchezaji wa Kagera Sugar, huku wachezaji wa Azam FC, Aggrey Morris na Peter Paul wakifungiwa na kupigwa faini kwa kosa kama hilo, huku Yanga ikipigwa faini ya Sh milioni 3.

 

Nyota hao wameadhibiwa baada ya Kamati ya Saa 72, kuwakuta na hatia kwenye michezo ya ligi ambayo imechezwa hivi karibu. Taarifa za kufungiwa wachezaji hao na faini mbalimbali kwa klabu zimetolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

 

Wachezaji wote hao wamefungiwa mechi tatu na faini ya Sh laki tano. Mbali na hao, Yanga imetozwa faini ya Sh. 3,000,000 (milioni tatu), kutokana na timu hiyo kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi katika mechi hiyo iliyofanyika Aprili 4, 2019, katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara likiwa ni kosa la nne msimu huu. Huku Ndanda wakipigwa faini kwa kosa kama hilo ikitozwa Sh milioni 1.5.

 

Wakati huohuo, Namungo FC imepewa ushindi wa pointi tatu na mabao matatu baada ya Friends Rangers kugomea mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza uliofanyika Aprili 13, 2019, kwenye Uwanja wa Majaliwa, hivyo timu hiyo sasa imefikisha alama 43 na kupanda Ligi Kuu Bara kutokea Kundi A.

Stori na Martha Mboma,

Comments are closed.