TFF YAPIGA STOP MCHAKATO WA UCHAGUZI SIMBA

Baada ya kukamilika kwa zoezi la kurejesha fomu kwa wanachama mbalimbali waliochukua ili kugombea uongozi Simba, Shirikisho la Soka Tanzania Bara (TFF) limesimamisha mchakato wa uchaguzi huo.

 

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi (TFF), Revocatus Kuuli, amesema mchakato wa uchaguzi huo umegubikwa na mambo mengi ambayo hayajafuata taratibu rasmi.

 

Kwa mujibu wa Radio Magic FM, Kuuli ameeleza kuwa mojawapo ya mambo hayo ni ada ya uanachama kwa ngazi ya Uenyekiti pamoja na Wajumbe kutofautiana, jambo ambalo ni kinyume na matakwa ya klabu pamoja na TFF.

 

Mwenyekiti huyo amesema Simba walipaswa kutoza kiasi cha laki mbili pekee kwa wagombea nafasi ya Uenyekiti huku laki moja ikiwa kwa wajumbe lakini badala yake imekuwa tofauti.

 

Aidha, Mwenyekiti huyo amefunguka kwa kueleza uwezekano mchakato huo ukaweza kuanza upya baada ya kuonekana kuwa na tartibu ambazo si sawa na ilivyokuwa inatakiwa.

 

Tayari zoezi la kurejeshwa kwa fomu limekamilika na leo Jumatatu ilitakiwa zoezi la kufanya usaili lianze.
Loading...

Toa comment