Kartra

TFF Yasimamishaligi Kuu kwa Wiki Mbili

SHIRIKISHO la Soka Tanzania, (TFF) limefuta mchezo wa kirafiki kati ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars dhidi ya Kenya, ‘Harambee Stars’.

 

Mechi hiyo ilipaswa ichezwe leo jion Machi 18, jijini Nairobi ambapo tayari Machi 15, Stars iliambulia kichapo cha mabao 2-1 kwenye mchezo wa kirafiki. Mechi ya leo imefutwa kwa sababu ya msiba wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli.

 

Taarifa rasmi iliyotolewa na TFF kupitia kwa Ofisa Habari wa TFF, Cliford Ndimbo imeeleza kuwa Stars itaendelea kuweka kambi Kenya kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya kufuzu Afcon dhidi ya Equatorial Guinea.

 

 

Pia mechi zote za ndani nazo zitasimama kwa muda wa wiki mbili ili kuungana na Watanzania wote kuomboleza msiba wa Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli


Toa comment