The House of Favourite Newspapers

TFF Yatangaza Uchaguzi Mkuu Agosti 16, 2025 Jijini Tanga

RAIS wa Shirikisho la Soka Nchini Tanzania (TFF), Wallace Karia

Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inatangaza Uchaguzi Mkuu wa TFF utakaofanyika tarehe 16/08/2025 jijini Tanga.

Nafasi zinazogombewa ni Rais (Nafasi 1) na nafasi ya Wajumbe wa Kamati ya Utendaji (Nafasi 6)

Gharama za kuchukua fomu Nafasi ya Rais ni 500,000 na Shilingi 200,000 kwa Nafasi za Wajumbe wa Kamati ya Utendaji.

Fomu zitaanza kutolewa kuanzia siku ya Jumatatu tarehe 16 hadi 20/06/2025 saa 10 kamili jioni. Fomu zinapatikana Makao Maku ya TFF na kwenye tovuti ya TFF.