TFF YATEUA WAJUMBE WAPYA KAMATI ZA UCHAGUZI, NIDHAMU, RUFAA MAADILI

Kamati ya Utendaji iliyokutana Jumamosi, Oktoba 20,2018 Makao Makuu ya TFF yaliyopo Karume, Ilala jijini Dar es Salaam ilipitia masuala mbalimbali ikiwemo kuchagua wajumbe wa kamati ya Uchaguzi, Kamati ya Nidhamu na Rufaa Maadili.

Pia Kamati ya Utendaji imepitisha tarehe ya Mkutano Mkuu wa TFF wa mwaka ambao utafanyika Jijini Arusha, Desemba 29, 2018.

Aidha, kikao hicho cha Kamati ya Utendaji kimepitisha mabadiliko madogo kwenye kamati ndogo ndogo za TFF ambapo mabadiliko hayo yametokana na baadhi ya Wajumbe kujiuzulu na Wajumbe wengine kukabiliwa na majukumu mengi.

 

MABADILIKO YA KAMATI ZA  TFF YAPO HAPA CHINI

KAMATI YA UCHAGUZI

1. MALANGWE ALLY -Mwenyekiti

2. MOHAMED MCHENGELA  -M/Kiti

3. BENJAMINI KARUME   –  Mjumbe

4. MOHAMED GOMBATI  –  Mjumbe

5. HAMISI ZAYUMBA  – Mjumbe

 

KAMATI YA NIDHAMU

1. KIOMONI  KIBAMBA – Mwenyekiti
2. PETER HELLA – M/Mkiti
3. KASSIM DAU – Mjumbe
4. HANDLEY MATWENGA – Mjumbe
5. TWAHA MTENGERA – Mjumbe

 

KAMATI YA RUFAA MAADILI

1. RICHARD MBARUKU – Mwenyekiti

2. THADEUS KARUA  -M/Kiti

3. MUSSA ZUNGU -Mjumbe

4. ASP BENEDICT NYAGABONA-Mjumbe

5. LUGANO HOSEA -Mjumbe

BREAKING: LEMA alivyotinga Polisi leo, Ishu ya ‘Mo Dewji’

Loading...

Toa comment