The House of Favourite Newspapers

TFF Yawapa Wawili Nafasi ya Manji Yanga

KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) imempitisha Baraka Igangula na Jonas Tiboroha kugombea nafasi ya Uenyekiti kwenye uchaguzi wa Yanga huku ikimkata Erick Minga kutokana na mkanganyiko kwenye taarifa zake.

 

Nafasi ya Makamu mwenyekiti wagombea waliopitishwa ni Titus Osoro,Pindu Luhoyo na Salum Magege Chota wakati Mgombea mmoja Yono Kevela ameenguliwa kwa matakwa ya kikatiba.

 

Nafasi ya Ujumbe waliopitishwa ni Athanas Kazighe,Ramadhan Said, Salim Rupia, Dominic Francis,Shafii Amri, Benjamin Mwakasonda,Christopher Kashiririka,Ally Msigwa,Silvester Haule,Arafat Haji,Frank Kalokole na Said Kambi.

 

Wagombea Wanne wameshindwa kufika kwenye usaili Hamad Islam,Seko Kongo,Leonard Marango na Benard Mabula kwa mujibu wa kanuni wameenguliwa katika uchaguzi.

 

Wagombea ambao hawajapitishwa wanayo haki ya kukata rufaa kwenye Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF.

Comments are closed.