The House of Favourite Newspapers
gunners X

TGNP YAFUNGA SIKU TANO ZA MAFUNZO YA URAGHBISHI

0
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa kijinsia Tanzania (TGNP) Lilian Liundi akizungumza wakati wa semina hiyo

Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) imefunga mafunzo ya Uraghbishi yaliyofanyika kwa muda wa siku tano ili kuwafunza na kuwajengea uwezo wanawake katika swala zima la utengaji wa bajeti yenye mrengo wa kijinsia.

Katika mafunzo hayo ya URAGHBISHI ambayo yenye maana ya kujua mchakato wa bajeti, ujenzi wa nguvu ya pamoja, ushiriki katika maswala ya kijamii, kujenga uwezo katika swala zima la mrengo wa kijinsia.

Akizungumza mapema leo wakati wa semina hiyo ambayo imefanyika katika viwanja vya TGNP Mabibo, Dar es Salaam, mratibu kutoka Idara ya mafunzo, Anna Sangai amesema kuwa wao kama TGNP wanatambua kwamba mtu yeyote wanae fanya nae kazi ana kitu na wao wana kitu hivyo basi vinaunganishwa ili kutengeneza kitu ambacho kitakwenda kutatua changamoto kwa jamii husika.

Ofisa Program Idara ya Habari na Mawasiliano, Jackson Malangalila akielekeza jambo katika mafunzo hayo

“Tumekuwa na siku tano za mafunzo na washiriki wametoka sehemu mbalimbali ikiwemo Kinondoni, Kitunda, Kivule na Majohe na tupo hapa ili kuwajengea uwezo wanawake katika swala zima la utengaji wa bajeti yenye mrengo wa Kijinsia, tunawajenga waweze kuchambua ili wakitoa mapendekezo iweze kuwanufaisha katika jamii zao.

” Na madhumuni hasa ya TGNP pamoja na kuwa sisi ni wataalam wa maswala ya kijamii wao ndio wataalam zaidi kwa kuwa wao ndio wanajua changamoto zilizopo katika maeneo yao kwa hiyo wao waongoze hiyo mikakati ili sisi tuweze kujifunza kwa kuwa wao ndio wanaelewa kuhusu sera itayotolewa inawanufaishaje au haiwanufaishi kwa hiyo sauti zao ndio zisikike kwa sababu wao wakishirikiana na jamii ndio wanajua vile wanavovihitaji katika maeneo yao kama vile maji, hospitali za kujifungulia na vinginevyo.

“Kwa hiyo tumewajenga ili wao wakienda katika huko kwenye ngazi ya jamii na watatoa viongozi ambao watakuwa wakishirikiana na jamii ili wananchi waweze kushiriki vizuri kwenye michakato ya maendeleo yao, ” amesema.

Washiriki wakiwa katika makundi kujadili mambo yaliyozungumziwa wakati wa semina hiyo

Nao washiriki wa mafunzo hayo wameeleza jinsi ambavyo semina hiyo imewasaidia akiwemo Zahara Omary kutoka katika kituo cha taarifa na maarifa cha kivule amesema kuwa atakwenda kuwawezesha wanajamii kutoka katika hali fulani na hali fulani.

” Napenda kuwashukuru TGNP kwa sababu nimejifunza vitu vingi ambavyo nitakwenda kurudisha kwenye jamii kwa sababu jamii haitambui nini maana ya bajeti yenye mrengo wa kijinsia sasa nitakwenda kuwaelimisha kuwa bajeti huwa inatengwa kwa ajili ya kutatua changamoto zao ambazo zipo katika jamii yao kinachotakiwa ni wao wasikae kimya wasema kama wana changamoto gani ili iweze kutatuliwa.

“Vile vile nilikuwa nikijua kwamba TGNP huwa wanajishughulisha na ukatili wa kijinsia tu kumbe wana vitu vingi ambavyo kwa upande wangu nimepata elimu yangu nitaitumia kwenda kuwaamasisha wanajamii ili waweze kutambua na watoe ushirikiano wa kusema vile ambavyo wanavyo na wanaelewe kuwa ni wajibu wa kila mwanajamii kuitambua bajeti yenye mrengo wa kijinsia, ” amesema.

Leave A Reply