The House of Favourite Newspapers

The Game, Lloyd Banks wamaliza bifu, 50 Cent achukia

0

50-Cent-The-Game-Lloyd-Banks
NEW YORK, Marekani
MEMBA wa zamani wa Kundi la G Unit, The Game, ameonekana kulimaliza bifu lake na aliyekuwa memba mwenzake ambaye bado yupo kwenye Lebo hiyo, Lloyd Banks baada ya kutupia picha wakiwa pamoja huko Dubai lakini katika hali ya kushangaza, staa 50 Cent ameonekana kutofurahishwa.

The Game na Lloyd Banks walikutana Dubai hivi karibuni na kupiga picha ambayo waliitupia kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram na kuandika “Still”, yaani bado.

Kitendo cha wawili hao kupatana kimeonekana kutomfurahisha 50 Cent ambaye ndiye kiongozi mkuu wa G Unit kwani hana maelewano mazuri na The Game.

50 Cent aliiposti picha hiyo na kuandika kwenye Instagram: “Unaona nini ukiiangalia hii picha? Naona kama mkanganyiko tu. Sitaki matatizo na sina tatizo na hawa wawili kufanya hivi, ila kuna washkaji ambao hawatapenda hii.”

Leave A Reply