The House of Favourite Newspapers

The Kadashians: Familia ‘Tata’ Lakini Maarufu Zaidi

Familia ya akina Kardashian.

FAMILIA ya akina Kardashian inatajwa kuwa ni moja ya familia yenye mastaa wengi ndani yake kwa sasa huku skendo ndiyo njia pekee inayodaiwa kuipelekea familia hiyo kuwa maarufu zaidi huku mwanadada mrembo Kim Kardashian akiwa ndiyo alama ya familia hiyo.

Robert Jr.

HISTORIA YAKE Familia hii inaanzia kwa mwanamama Kris na mumewe Robert Kardashian ambao walioana mwaka 1978 na wawili hao wakazaa watoto watatu ambao ni Kourtney, Kim, Khloe wa mwisho akiwa ni Robert Jr.

Mwaka 1990, mapenzi ya Kris na Robert yaliingia dosari na wawili hao wakamwagana ambapo Bruce Jenner (kwa sasa Caitlyn Jenner baada ya kubadili jinsia na kuwa mwanamke) alimuoa Kris na pamoja wakazaa watoto wawili ambao ni Kendall Jenner na Kylie Jenner ingawa Bruce kabla ya hapo alipitia ndoa mbili na kuzaa watoto wengine ambao hawahusishwi na familia ya kina Kardashian kabisa.

Hivyo basi kutokana na mchanganyiko huo familia ya Kardashian inawajumuisha:- Kim, Kourtney, Khloe, Robert Jr, Kendall, Kylie, Kris na Bruce. UMAARUFU WAO KIM ARDASHIAN Umaarufu wa familia hii unatokana na vituko mbalimbali vinavyofanywa na akina Kardashian ambapo awali ilianza kwa skendo ya video ya ngono ‘sex tape’  liyovuja ikimuonesha Kim Kardashian akingonoka na mwanamuziki Ray J.

Baada ya hapo mwanadada huyo akawa maarufu zaidi na kutengeneza ‘profile’ yake kwa kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na mastaa kibao wa kiume ambapo madai ya kutengeneza shepu yake na kuwa gumzo zaidi yaliibuka.

maarufu wa shepu ya Kim Kardashian ukasababisha mapaparazi nchini Marekani waivumbue na familia yake kwa ujumla ambapo warembo wengine ambao ni dada wa Kim Kardashian, Kourtney, Khloe, Kendall na Kylie bila kusahau mtoto pekee wa kiume Robert Jr, wakagunduliwa jambo lililosababisha kufanyiwa kipindi cha televisheni, Keeping Up with the Kardashians ambacho kwa sasa ni maarufu sana huku kupitia umaarufu huo Kim akipata dili za fasheni na kupiga picha nyingi za matangazo mbalimbali.

Umaarufu wa familia hii uliendana pia na kuingia kwa mkali wa Hip Hop, Kanye West kwenye listi ya wanaume waliowahi kutoka na Kim ambapo jamaa alionekana kukolea zaidi kiasi cha kutangaza ndoa na kuoana moja kwa moja huku wakipata mtoto, North West na wanatarajia mtoto mwingine hivi karibuni.

KHLOE KARDASHIAN Wakati Kim akiendelea kuwa maarufu na kuongeza idadi ya mashabiki zake hasa kupitia skendo zake kama vile kujiachia utupu kwenye majarida, mdogo wake ambaye ni Khloe naye hakusalimika na yombo vya habari ambapo alianza kuripotiwa kutembea na staa wa kikapu Lamar (kwa sasa wameachana) ambapo uhusiano wao ulikuwa na mvuto wa kipekee.

KENDALL JENNER, KYLIE JENNER NA ROBERT JR. KARDASHIAN Kama hiyo haitoshi, Kendall Jenner ambaye ni mwanamitindo amekuwa akiandamwa na skendo kadhaa za kutoka na dogo anayekimbiza kwenye muvi Hollywood, Orlando Bloom huku Kylie Jenner akiwa kwenye penzi zito na mkali wa Hip Hop, Tyga. Kaka yao ambaye ni Robert Jr.

Amekuwa akihusishwa na utumiaji wa madawa ya kulevya, kupigana na wanahabari lakini kubwa zaidi ikiwa ni skendo ya kukuwadiwa mwanadada Selena Gomez na mama yake lakini hata hivyo mchongo huo ulidunda baada ya madai kuwa Selena alimchomolea mshkaji.

CAITLYN JENNER Wakati watoto wapo mbele kutengeneza vichwa vya habari, familia hiyo ilitikisa zaidi baada ya baba wa familia, Bruce Jenner kutangaza kubadili jinsia na kuwa mwanamke; pengine suala hilo likiwa moja ya vituko vikubwa kuwahi kufanyika kwa mtu maarufu kama huyo duniani.

KRIS JENNER Funga kazi wa familia hii ni mwanamama, Kris ambaye baada ya mumewe Bruce kubadili jinsi yake naye ameamua kusaka pumziko la moyo wake ambapo ameripotiwa kutoka na meneja wa masuala ya muziki, Corey Gamble (34) ambaye ni kama mwanaye kiumri kutokana na kumzidi kwa takriban miaka 25.

Comments are closed.