The House of Favourite Newspapers

Thea Ataja Madhara ya Mapedeshee

GLADNESS MALLYA | RISASI JUMAMOSI | DAR ES SALAAM

STAA wa filamu nchini, Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ amefunguka kuwa hana mpango na hategemei mapedeshee  kuendesha maisha yake kwani madhara yake ni makubwa.

Akibonga na Risasi Jumamosi, Thea alisema katika maisha yake hajawahi kutegemea wanaume mapedeshee wamwendeshee maisha yake kwani kuna hasara kubwa kwa sababu mastaa wengi wa kike wanaoishi kwa kuwategemea hujikuta wakiachwa na kurudi chini kabisa hivyo ni funzo kubwa.

“Siwezi na sijawahi kutegemea mapedeshee kuendesha maisha, mastaa wa kike wengi tumewaona wakiendesha magari ya thamani, wakiishi kwenye nyumba nzuri lakini wanapoachwa wananyang’anywa kila kitu, wanafilisika wanarudi chini, mimi tangu nimetengana na Mike Sangu sijawahi kumwanika mwanaume yeyote kwamba ni mpenzi wangu,” alisema Thea.

Comments are closed.