THEA: NABEBA MIMBA ILI NDOA IVUNJIKE

Ndumbagwe Misayo ‘Thea’

NI kama kicheke­sho lakini ni kweli; Staa wa Bongo Muvi, Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ amesema anabeba mimba ya mwanaume mwingine ili ndoa kati yake na mumewe Michael Sangu ‘Mike’ ivunjike rasmi kanisani.

Akizungumza na Za Motomoto News, Thea alisema utaratibu wa ndoa za Kikristo hautambui talaka ndiyo maana tangu amemwagana na mumewe hajaolewa kwa sababu ya kifungo hicho cha sheria za dini ambapo sasa ameamua ‘kujilipua’ ili apate mume mwingine.

“Unajua kanisani kama mmetengana na mume halafu ukaenda kuzaa na mwanaume mwingine ndoa inakuwa imeshavunjika tayari, sasa hivi nina mpenzi na ninataka nibebe mimba yake; hapo ndiyo ndoa na Mike itakuwa imefikia ukingoni,” alisema Thea.

Loading...


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment