The House of Favourite Newspapers

Thea: Tutukaneni, Tunatetea Haki Yetu

0

 

Stori: Gladness Mallya | RISASI JUMATANO | Za Motomoto News

MSANII wa filamu za Kibongo, Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ ameibuka na kuwabeza watu wanaowaponda waigizaji kwa kitendo chao cha kuandamana kupinga uuzwaji holela wa sinema za nje kwa kuwaambia waendelee kutukana kwani wao walifanya hivyo ili kutetea haki yao.

Akipiga stori na Za Motomoto News, Thea alisema wao walifanya hivyo kwa kuona inafaa, sasa kama kuna watu wengine wanatoa maneno machafu juu yao watakuwa na lao jambo kwa sababu hata Hollywood ilifi ka kipindi tasnia ikasimama kabisa.

“Ninachoweza kusema ni tumuombe Mungu hekima yake ituangalie, tujitathmini pale tulipoanguka tuparekebishe, wanaotukana waendelee kutukana lakini mimi fi lamu ndiyo inayoniweka mjini, nakula, nalala na kuvaa kwa kazi hiyo,” alisema Thea.

Leave A Reply