The House of Favourite Newspapers

Tiba ya kisukari-5

0

kisukariBaada ya kuelezea kwa kirefu tiba ya kisukari, leo tunamalizia hivyo ungana nani ili uelimike zaidi.

Kuna faida nyingine kubwa zaidi ya kutumia majani ya mpapai ambayo yana uwezo mkubwa wa kutibu vidonda vitokanavyo na kisukari kwa haraka.

Waganga wengi wa tiba asili kutoka Japani na Australia na wengine wengi kutoka mataifa mbalimbali, wamekuwa wakitumia majani ya mpapai kutibu kisukari kwa miaka mingi sasa.

Mahitaji:

  • Majani 10 ya mpapai
  • Maji lita 2

Maandalizi:

  • Tumbukiza majani hayo ya mpapai katika maji.
  • Yachemshe katika maji ya moto hadi yatakapobaki nusu yake (lita 1).
  • Ipua na uache yapowe
  • Kunywa maji haya kidogo kidogo kutwa nzima. Fanya hivi kwa mwezi mmoja mpaka miwili.

Juisi hii ya majani ya mpapai iliyoandaliwa kwa mtindo huu ni nzuri katika kuondoa sumu mwilini na kurekebisha afya yako kwa ujumla huku ikirekebisha matatizo katika mfumo wa umeng’enyaji wa chakula na kuongeza kinga ya mwili wako.

Mpenzi msomaji, nafikiri utakuwa umepata darasa la kutosha kuhusiana na tiba ya maradhi ya kisukari ambayo yamekuwa yakiwasumbua watu wengu hivi sasa.

Leave A Reply