The House of Favourite Newspapers

Tiba ya Wasiwasi ‘Anxiety’

0

Watu wengi wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo la kupatwa na wasiwasi lakini huwa hawajui kinachosababisha na jinsi ya kuondoa tatizo hilo.
Leo nimeamua kuwaletea tiba mbalimbali ya tatizo hilo

Chai ya kijani ‘Green Tea’
Kama unajihisi una wasiwasi, unashauriwa kunywa chai ya kijani, inasaidia kuondoa hali hiyo haraka sana.
Chai ya kijani imesifika kwa kutuliza mapigo ya moyo, Wajapani wamethibitisha hilo  kwa kufanya uchunguzi ambao umedhihirisha kuwa chai hiyo ina uwezo mkubwa wa kumaliza tatizo hilo.

Nanaa
Ni tiba ambayo imekuwa ikitumika kwa muda mrefu na Wagiriki kwa ajili ya kuondoa wasiwasi, pia husaidia mtu kupata usingizi na kujipumzisha.
Watu wengi hushauriwa kutumia kwenye chai na wakati mwingine hutumika kwenye vidonge na tincture ya kuweka kwenye vidonda.

Mazoezi
Mazoezi kwa wingi pia husaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa wasiwasi, pale utakapohisi una wasiwasi mwingi, jichukulie kama hali ya kawaida fanya mazoezi ya mwili.

Mrujuani
Ni tiba nyingine ambayo inasaidia kuondoa wasiwasi.

Ukihisi wasiwasi, kula kitu haraka
Kama unahisi wasiwasi unatakiwa kula kitu haraka sana kwa sababu wasiwasi ni dalili kubwa ya kupungua kwa sukari mwilini, dalili za ugonjwa wa wasiwasi mara nyingi mtu hujikuta ana hasira sana.

Kitu cha kunywa ukihisi wasiwasi
Chokleti nyeusi, chai ya moto, upande wa chakula unaweza kula chakula chochote kwa wakati huo ili kurudisha sukari kwenye hali yake.

Leave A Reply