The House of Favourite Newspapers

Tiboroha Kusubiria Wapya Uchaguzi Yanga

Mgombea wa nafasi ya uenyekiti ndani ya Yanga, Dk Jonas Tiboroha (katikati).

MGOMBEA wa nafasi ya uenyekiti ndani ya Yanga, Dk Jonas Tiboroha na wagombea wenzake wa awali, wanasubiria maamuzi ya kamati ya rufaa za uchaguzi ya TFF ili kuwajua wapinzani wao kwa ajili ya kuanza mchakato wa kuwania nafasi mbalim bali za uongozi ndani ya klabu hiyo.

 

Yanga kwa sasa ipo katika mchakato wa kufanya uchaguzi mkuu wa klabu hiyo Mei 5, mwaka huu kwa kuziba nafasi zote zilizo wazi ambapo kwa sasa wanasubiria rufaa iwapo wagombea walioenguliwa watafanya hivyo ili kupeleka majina hayo katika Kamati ya Maadili ya TFF kisha kuwaunganisha.

 

Kamati ya Uchaguzi ya TFF hivi karibuni iliwaengua baadhi ya wagombea akiwemo aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Klabu ya Yanga, Hussein Nyika kutokana na kutokidhi vigezo.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Malangwe Mchungahela amesema kuwa, kwa sasa bado wanasubiria tarehe ya kukata rufaa ifike ili kujua waliokata rufaa na kujua wafanye nini na iwapo ikitokea hakutakuwa na mtu wa kufanya hivyo majina hayo yatapelekwa katika kamati ya maadili kisha watakaopitishwa ndiyo watakaoungana na kina Tiboroha.

 

“Wagombea wa mwanzo wanatarajia kuungana na wenzao mara baada ya Kamati ya Maadili ya TFF kupitia majina yote ya wagombea na ndipo tutakapowajumuisha wote watakaoingia katika kinyang’anyiro hicho,” alisema Mchungahela.

STORI NA KHADIJA MNGWAI | CHAMPIONI IJUMAA

Comments are closed.