The House of Favourite Newspapers

TID: kurejesha heshima!

0

tid

BAADA ya kubamba na Ngoma ya Kibakubaku,  Khaleed Mohamed ‘TID’ amesema kuwa kwa sasa yuko ‘chimbo’ akijiandaa kuja na vitu adimu ambavyo anaamini atarejesha heshima katika soko la muziki wa Bongo Fleva.

Akichezesha mdomo na Centre Spread, TID alisema kwa muda mrefu amekuwa akiusoma muziki na kuamua kujipanga upya ili arejee kwenye enzi zake za ‘Nyota Yako’ huku akijipambanua kuwa amewa-miss  wapenzi na mashabiki wa kazi zake.

“Niko chimbo kwa sasa, nilitulia kidogo ili niusome mchezo mzima wa gemu, nataka kurejesha heshima yangu ya enzi za Nyota Yako na Asha, mimi ni mfalme katika muziki, niko vizuri na ni kipaji changu halisi, sibahatishi,” alisema TID.

Leave A Reply