The House of Favourite Newspapers

TID, MZAZI MWENZIYE PACHIMBIKA!

DAR ES SALAAM: Mambo siyo poa kwa wazazi wa binti aitwaye Tania, Khaleed Mohamed ‘TID’aliye mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva na mama mtoto wake Shekha Mdogo a.k.a Miss Small Shekha.

 

Wawili hao wameingia kwenye mvutano baada ya kila mmoja kutoa msimamo tofauti kuhusu unasaba wa mtoto wao huyo, ambapo TID anasema ni mtoto wake, wakati mama mtu akikanusha vikali.

SHEKHA ALIANZISHA

Shekha ambaye kwa sasa anaishi Ujerumani, ndiye alikuwa wa kwanza kuwasiliana na paparazi wetu, akasema anachukizwa na namna TID anavyotangaza kuwa mtoto huyo ni wake, wakati siyo kweli.

“Unajua huyu TID nahisi hayo madawa anayotumia (hajafafanua ni dawa za nini) yameshaanza kumuharibu, huyu mtoto sio wake kwa sababu nilishapima mpaka DNA na baba mzazi wa mtoto huyu ambaye makazi yake yapo hukohuko Bongo na majibu yakaonesha kwamba mtoto sio wa TID sasa kinachomfanya amng’ang’anie ni nini?” alihoji Shekha na kuongeza: 

“Kiukweli mimi ninachoomba TID amtoe kabisa huyu mtoto akilini mwake, kwa sababu kwanza mwanangu hajui hata kama ana baba anaitwa TID na tulishaondoka huko Tanzania tangu binti yangu akiwa na umri wa mwaka mmoja na miezi kumi… na sasa ana miaka mitatu, atakuwa ameshamsahau kabisa.”

 

TID HUYU HAPA

Amani pia lilifanya jitihada za kumtafuta TID na kufanikiwa ambapo baada ya kupatikana alisema anachokifahamu na hakitabadilika akilini mwake ni kwamba Tania ni mtoto wake.

“Huyu mwanamke ananishangaza sana, kwa sababu mimi ninachojua huyo mtoto ni wangu na mpaka kuondoka kwake hapa mimi ndio nilikwenda ubalozi kusaini ndio mtoto akapata Visa ya kusafiri. “Sasa simuelewi anavyosema nikae mbali na yule mtoto, isitoshe mimi nina mpaka ushahidi wa vyeti. Tania ni mwanangu na atabaki kuwa mwanangu siku zote,” alisema TID.

Stori: Memorise Richard, Amani

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.