The House of Favourite Newspapers

Tigo Hakupoi, Yaja Na Jipya: Sako kwa Bako

0

Afisa mkuu wa Biashara wa Tigo, Isaack Nchunda, akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa kampeni mpya ya Tigo iitwayo ‘Sako kwa Bako’ yenye lengo la kusherehekea mafanikio ya Tigo na wateja wake, kulia ni Mkurugenzi wa Masoko kutoka Tigo, Edwardina Mgendi.

Dar es Salaam, 22 Mei 2024. Tigo, Kampuni ya mtandao wa simu ya Tigo hapa nchini imekuja na uzinduzi wa kampeni yake mpya inayojulikana kama ‘Sako Kwa Bako’ ambayo inalenga sio tu kufufua uhusiano na wateja wake bali pia kuadhimisha hatua muhimu ya kufikia zaidi ya wanachama milioni 20.

‘Sako Kwa Bako’ inamaanisha “pamoja kila hatua ya njia,” ambayo inaonyesha dhamira ya Tigo ya kuboresha uhusiano wake na wateja kwa kuamsha kumbukumbu za thamani za uzoefu wa pamoja, kutoka kauli mbiu za kampeni maarufu hadi bidhaa na huduma zinazobadilisha maisha.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Tigo, Kamal Okba alisema, “Kwa ‘Sako Kwa Bako,’ tunasherehekea wateja wetu milioni 20 na kutoa shukrani kwa uaminifu wao usioyumba. Safari yetu imekuwa yenye utajiri mkubwa, ikijaa uvumbuzi na bidhaa na huduma nyingi za kwanza sokoni pamoja na huduma bora kwa wateja kwa bidii kuhakikisha kila mteja wa Tigo anahisi kuunganishwa, kuthaminiwa, na kuwezeshwa.”

Akitoa maoni yake kuhusu mafanikio haya, Afisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Isack Nchunda alihusisha ukuaji wa idadi ya wateja na utamaduni wa Tigo unaomlenga mteja, akisema, ” Tigo, tumejitolea kuendesha mabadiliko ya kidijitali nchini Tanzania.

Picha ya pamoja baada ya uzinduzi.

Kwa mtandao wetu unaotambuliwa kimataifa kuwa na kasi zaidi nchini Tanzania, tunapiga hatua kubwa kwa kueneza huduma ya 4G  nchini kote, iliyopangwa kukamilika ifikapo Juni 2024. Zaidi ya hayo, tumeanzisha teknolojia ya 5G yenye kasi zaidi katika miji mikuu na sisi ni kampuni ya kwanza ya mawasiliano kutoa huduma za nyumbani na ofisini za Fiber.”

‘Sako Kwa Bako’ inaimarisha ahadi ya Tigo ya kutoa huduma na bidhaa za kidijitali na kifedha zilizobinafsishwa huku ikikuza kampeni na matangazo yenye athari kubwa yanayoboresha maisha ya wateja kote nchini.

Uzinduzi huu unaashiria hatua ya kusisimua katika safari ya Tigo kuelekea kuboresha mawasiliano na uzoefu wa kifedha wa wateja nchini Tanzania. Tunawahimiza wateja wote kutembea nasi tunapowasha tena uzoefu wa kukumbukwa kupitia kampeni ya ‘Sako Kwa Bako’.

Leave A Reply